Ijumaa, 24 Oktoba 2014

WATU WA JAMII YA KIMASAI WAGOMEA MIPANGO MIJI

Ni wale waishio Bagamoyo

watu wa jamii ya kimasai ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya chamakweza katika kata ya pera wilaya ya bagamoyo mkoa wa Pwani.wamepinga vikali hatua za serikali kukigawa kijiji hicho kwa matumizi mengine wakati awali eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo na si kwa ajili ya matumizi mengine.wakazi hao wamekubaliana kwa pamoja kukataa agizo hilo la serikali kwani kama watakubaliana na rai hiyo watapoteza eneo lao ambalo sehemu kubwa imetengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo.kijiji cha chamakweza kilitengwa na serikali tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini kwa ajili ya matumizi ya mifugo,na wakazi wa chamakweza ambao wengi wao ni wafugaji wana ngombe jumla yao ni 22,000, mbuzi 6,000, kondoo 4,000.kwa kuwa eneo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo yana mazingira mazuri ya kuchunga wanyama wao.eneo la chamakweza mbala na pingo ni maeneo ambayo yana nyasi zenye rutuba ambazo wanyama hupata malisho bora hapo changamoto pekee iliyokuwepo ni uharibifu wa wa mazingira hasa katika maeneo ya Ruvu darajani ambapo eneo hili linatumika sana na watu wa jamii ya kifugaji hasa kutoka maeneo ya bara mikoa ya Shinyanga,Taborana Mwanza.wengi wa wafugaji wanapinga mpango huo kwani utawalazimisha kufuga kisasa na hivyo kupunguza idadi ya mifugo na kutunza mazingira jambo ambalo ni kinyume sana na wafugaji na matakwa yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni