BLOG HII INAHUSU UTUNZAJI WA MAZINGIRA. TUYALINDE MAZINGIRA YASAIDIE KWA VIZAZI VYA BAADAE.
Jumapili, 26 Oktoba 2014
ZANZIBAR KULINDA MAZINGIRA
Mazingira ya bahari
wavuvi wa vijiji mbalimbali vya unguja hasa mikoa ya kusini wmehimizanz kutunza mazingira na kulinda hasa ya bahari na kuachana na uvuvi haramu ambao ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira na rasilimali za bahari.Kwani kwa kuto kutunza mazingira yetukuna athari kubwa itatokea ikiwepo upungufu wa samaki na mazalia yake na uharibifu wa matumbawe.Baadhi ya vijiji vya Marumbi na Chwaka zimepungua samaki kwa kiasi kikubwa tangu mnamo mwaka 2012 mpaka 2014.serikali ya Zanzibar imetenga maeneo tofautitofauti kwa ajili ya uvunaji wa samaki pomoja kufungua masoko ya kisasa kwa ajili uuzaji wa mazao ya samaki kisasaMto wami
Ni mrefu kwa kina
Mto wami ni mto unaopatikana kuanzia mkoa wa Morogoro umepita katika wilaya tofauti mpaka kumwaga maji yake katika wilaya ya Bagamoyo mkoa wa pwani.kutokana kuwa na mazingira mazuri wenyeji wengi ambao wanapakana na mto huu wamekuwa wanajihusisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji kutokana na uwepo wa fursa za uzalishaji mali kutokana na uwepo wa mto huu.Mto wami pia hutumika katika shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambao kimsingi mto huu ni muhim u sana kwa uzalishaji mali na usafirishaji
Ijumaa, 24 Oktoba 2014
WATU WA JAMII YA KIMASAI WAGOMEA MIPANGO MIJI
Ni wale waishio Bagamoyo
watu wa jamii ya kimasai ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya chamakweza katika kata ya pera wilaya ya bagamoyo mkoa wa Pwani.wamepinga vikali hatua za serikali kukigawa kijiji hicho kwa matumizi mengine wakati awali eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo na si kwa ajili ya matumizi mengine.wakazi hao wamekubaliana kwa pamoja kukataa agizo hilo la serikali kwani kama watakubaliana na rai hiyo watapoteza eneo lao ambalo sehemu kubwa imetengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo.kijiji cha chamakweza kilitengwa na serikali tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini kwa ajili ya matumizi ya mifugo,na wakazi wa chamakweza ambao wengi wao ni wafugaji wana ngombe jumla yao ni 22,000, mbuzi 6,000, kondoo 4,000.kwa kuwa eneo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo yana mazingira mazuri ya kuchunga wanyama wao.eneo la chamakweza mbala na pingo ni maeneo ambayo yana nyasi zenye rutuba ambazo wanyama hupata malisho bora hapo changamoto pekee iliyokuwepo ni uharibifu wa wa mazingira hasa katika maeneo ya Ruvu darajani ambapo eneo hili linatumika sana na watu wa jamii ya kifugaji hasa kutoka maeneo ya bara mikoa ya Shinyanga,Taborana Mwanza.wengi wa wafugaji wanapinga mpango huo kwani utawalazimisha kufuga kisasa na hivyo kupunguza idadi ya mifugo na kutunza mazingira jambo ambalo ni kinyume sana na wafugaji na matakwa yao.
BARAZA LABARIKI UWANJA SERENGETI
NEMC WARIDHIA UWANJA
Baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira limeridhia ujenzi wa uwanja wa ndege kujengwa katika mbuga ya serengeti kutokana na kuwa na uwanja mdogo wa ndege ambao haukidhi haja ambao unapatikana kilometa kama arobaini hivi kutoka mjini serengeti kwa kuwa sehemu kubwa ya wilaya ya serengeti imebwana mbuga hii itakuwa fursa kubwa wakazi wa eneo hili kupata ajira ambao ni kilo kikubwa kwa wakazi wa wilaya ya serengeti.Lakini changamoto kubwa iliyokuwepo mbele ya jamii ni kutunza uwanja huu kwa ajili ya usafifi na italiiUZURI WA MSITU WA JOZANI ZANZIBAR
mandhari ya jozani
msitu wa jozani unapatikana kilometa takribani sitini kutoka katikati ya mji wa Unguja kuelekea kaskazini mwa mji huo.Ni msitu ambao una mandhari nzuri sana kutokana na uoto wa asili na unavutia mno kuangalia.Pia kuna udongo wenye rutuba sana na mazingira mzuri ya uwekezeji na kuvutia watalii ambao huenda Zanzibar kwa wingi kwa ajili ya kutembelea kivutio hicho kwa ajili ya kujionea mazingira jinsi yalivyo
MAAJABU YA MSITU WA JOZANI
MOJA YA MAAJABU YA JOZANI
Msitu wa jozani ni msitu unaopatikana takribani kilometa sitini kutoka katikati ya mji wa mji wa unguja ni moja ya misitu mikubwa inayopatikana katika visiwa vya bahari ya hindi humo wanapatikana kima wekundu ambao hawapatikani mahali popote pale duniani isipokuwa zanzibar pekee
kima wekundu nikivutio kikubwa katika msitu huo ambao kwa asili kima hao ni wasumbufu wa kuharibu mazao ya wenyeji wa maeneo yanayozunguka lakini ukiacha matatizo hayo msitu huo ni wenye mandhari nzuri sana na yakuvutia
lakini msitu huo umekuwa ni sehemu mkubwa ambayo watalii hutembelea na kuongeza pato la taifa
Jumanne, 7 Oktoba 2014
SAFU YA MILIMA YA UDZUNGWA
Moja ya manzari nzuri
yenye kuvutia katika ardhi ya Tanzania ni kuwepo safu ya milima ya Udzungwa
ambayo kimsingi milima hiyo imekuwepo hapo tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwenguni .
kinachoshangaza zaidi ni ile hali ya safu kujipanga vizuri
tangu mwanzo wa mkoa wa Morogoro mpaka mkoani Iringa.
Milima ya Udzungwa
imepambwa na uoto wa kijani wenye kuvutia mno
na safu za miti zilizojipamba kiajabu mno kuzunguka karibu sehemu kubwa
ya wilaya ya Ifakara na maeneo ya kidatu katika mkoa wa Morogoro.
Safu ya milima ya Udzungwa pia wanapatikana wanyama wadogo
wadogo kama vile nyani sokwe tumbili mbweha
na wanyama wengine .Na hivyo kuendelea kupendezesha mandhari na kuvutia
watalii wa ndani nan je ya nchi.
Ni vema kila mdau wa mazingira akafahamu namna ya kuyatunza na kuenzi mazingira yaliyo mzunguka lengo na makusidio
kwa ajili vizazi vyetu vyote.
Kutokana na maliasili zilizokuwepo kwenye nchi yetu ni vemaq
tukatumia kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi yetu kwani umasikini uliokithiri ni matokeo ya
mabaya ya matumizi ya rasilimali.
zi mabaya ya matumizi ya nishati mbadakla na matumizi
mengine ya kilimo mkwa ajili ya wananhi kujiongezea kipato chao katika ilim
kujikimu kimaisha.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)