Jumapili, 26 Oktoba 2014

MJI WA LUSHOTO

HISTORIA FUPI YA MJI WA LUSHOTO

 Lushoto ni mji mdogo uliopo kwa kimo cha mita 1930 juu ya usawa wa bahari kwenye milima ya usambara ni makao makuu ya wilaya ya lushoto.mji ulianzishwa kwea jina la wilhelmstal wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya mashariki jina hilo lilitolewa kwa heshima yakaisar wilhelm aliyekuwa mtawala wa ujerumani hadi mwka 1918.kuna barabara ya lami inayounganika na barabara kuu ya Arusha na dar es salaa.mazingira ya wilaya ya Lushoto ni nzuri na baridi ya wastani wenyeji wa wilaya ya Lushoto wengi wao ni wasambaa ,wazigua ,wabondei ambao hujishughulisha sana na shughuli za kilimo kuendesha maisha yao.

ZANZIBAR KULINDA MAZINGIRA

Mazingira ya bahari

wavuvi wa vijiji  mbalimbali vya unguja hasa mikoa ya kusini wmehimizanz kutunza mazingira  na kulinda hasa ya bahari na kuachana na uvuvi haramu ambao ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira na rasilimali za bahari.Kwani kwa kuto kutunza mazingira yetukuna athari kubwa itatokea ikiwepo upungufu wa samaki na mazalia yake na uharibifu wa matumbawe.Baadhi ya vijiji vya Marumbi na Chwaka zimepungua samaki kwa kiasi kikubwa tangu mnamo mwaka 2012 mpaka 2014.serikali ya Zanzibar imetenga maeneo tofautitofauti kwa ajili ya uvunaji wa samaki pomoja kufungua masoko ya kisasa kwa ajili uuzaji wa mazao ya samaki kisasa

Mto wami

Ni mrefu kwa kina

Mto wami ni mto unaopatikana kuanzia mkoa wa Morogoro umepita katika wilaya tofauti mpaka kumwaga maji yake katika wilaya ya Bagamoyo mkoa wa pwani.kutokana kuwa na mazingira mazuri wenyeji wengi ambao wanapakana na mto huu wamekuwa wanajihusisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji kutokana na uwepo wa fursa za uzalishaji mali kutokana na uwepo wa mto huu.Mto wami pia hutumika katika shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambao kimsingi mto huu ni muhim u sana kwa uzalishaji mali na usafirishaji

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

WATU WA JAMII YA KIMASAI WAGOMEA MIPANGO MIJI

Ni wale waishio Bagamoyo

watu wa jamii ya kimasai ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya chamakweza katika kata ya pera wilaya ya bagamoyo mkoa wa Pwani.wamepinga vikali hatua za serikali kukigawa kijiji hicho kwa matumizi mengine wakati awali eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo na si kwa ajili ya matumizi mengine.wakazi hao wamekubaliana kwa pamoja kukataa agizo hilo la serikali kwani kama watakubaliana na rai hiyo watapoteza eneo lao ambalo sehemu kubwa imetengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo.kijiji cha chamakweza kilitengwa na serikali tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini kwa ajili ya matumizi ya mifugo,na wakazi wa chamakweza ambao wengi wao ni wafugaji wana ngombe jumla yao ni 22,000, mbuzi 6,000, kondoo 4,000.kwa kuwa eneo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya mifugo yana mazingira mazuri ya kuchunga wanyama wao.eneo la chamakweza mbala na pingo ni maeneo ambayo yana nyasi zenye rutuba ambazo wanyama hupata malisho bora hapo changamoto pekee iliyokuwepo ni uharibifu wa wa mazingira hasa katika maeneo ya Ruvu darajani ambapo eneo hili linatumika sana na watu wa jamii ya kifugaji hasa kutoka maeneo ya bara mikoa ya Shinyanga,Taborana Mwanza.wengi wa wafugaji wanapinga mpango huo kwani utawalazimisha kufuga kisasa na hivyo kupunguza idadi ya mifugo na kutunza mazingira jambo ambalo ni kinyume sana na wafugaji na matakwa yao.

BARAZA LABARIKI UWANJA SERENGETI

NEMC WARIDHIA UWANJA

Baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira limeridhia ujenzi wa uwanja wa ndege kujengwa katika mbuga ya serengeti kutokana na kuwa na uwanja mdogo wa ndege ambao haukidhi haja ambao unapatikana kilometa kama arobaini hivi kutoka mjini serengeti kwa kuwa sehemu kubwa ya wilaya ya serengeti imebwana mbuga hii itakuwa fursa kubwa wakazi wa eneo hili kupata ajira ambao ni kilo kikubwa kwa wakazi wa wilaya ya serengeti.Lakini changamoto kubwa iliyokuwepo mbele ya jamii ni kutunza uwanja huu kwa ajili ya usafifi na italii

BARAZALABARIKI UWANJA SERENGETI

 

UZURI WA MSITU WA JOZANI ZANZIBAR

  1. mandhari ya jozani

  2.  msitu wa jozani unapatikana kilometa takribani sitini kutoka katikati ya mji wa Unguja kuelekea kaskazini mwa mji huo.Ni msitu ambao una mandhari nzuri sana kutokana na uoto wa asili na unavutia mno kuangalia.Pia kuna udongo wenye rutuba sana na mazingira mzuri ya uwekezeji na kuvutia watalii ambao huenda Zanzibar kwa wingi kwa ajili ya kutembelea kivutio hicho kwa ajili ya kujionea mazingira jinsi yalivyo