Jumatano, 17 Septemba 2014

Tunza mazingira yakutunze

Mazingira ni kile unachokiona au kile kinachokuzunguka kupitia maisha  yetu,ili mazingira yatututunze nasi pia tunafaa kuyatunza ili yatoe faida katika kizazi chetu na kizazi kijacho.kwa mfano leo katika jiji la Dar  es salaam kuna uharibifu mkubwa wa mazingira  hasa katikati  ya jiji.Unaweza ukakuta chupa za maji ya kunywa zilizotumika zimejaa uchafu wa haja ndogo na kutupwa honyo katikati ya barabara.Hata baada ya barabara zetu kuboreshwa na kuonekana safi muda wote bado jamii yetu inafikiri ni jukumu la halmashauri ya jiji kuboresha mazingira na usafi kwa jumla.Jamii yetu inatakiwa ibadilike kwani ni jukumu la kila mmoja kuboresha mazingira yanayomzunguka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni